Kampuni ya Acacia Mining PLC kupitia migodi yake ya Buzwagi na Bulyanhulu imeshiriki maonyesho ya Teknolojia Bora ya Uzalishaji Dhahabu kwa Maendeleo ya Kijamii na Uchumi wa Viwanda yanayofanyika katika viwanja vya Kalangalala Mkoani Geita.
Akizungumzia Ushiriki wa Migodi ya Acacia ya Bulyanhulu na Buzwagi Mhandisi wa Uchenjuaji wa Bulyanhulu Emmanuel Muchunguzi amesema katika Maonyesho hayo wamejipanga kuielimisha jamii kuhusu uchimbaji wa madini chini ya ardhi, hatua za Uchenjuaji wa Dhahabu, masuala ya Mazingira, Afya, na usalama mahala pa kazi.
Muchunguzi amewakaribisha wadau mbalimbali waweze kutembelea banda la Maonyesho la Acacia ili wajifunze masuala mbalimbali hasa ya kuhusu uchimbaji na Uchenjuaji salama kwani usalama ndiyo nguzo muhimu ya Uzalishaji wa Dhahabu. Maonyesho hayo yameandaliwa na Mkoa wa Geita.
ANGALIA PICHA HAPA
Wakazi wa Geita wakiwa katika banda la Kampuni ya Uchimbaji madini ya Acacia kwenye maonyesho ya Teknolojia Bora ya Uzalishaji Dhahabu kwa Maendeleo ya Kijamii na Uchumi wa Viwanda yanayofanyika katika viwanja vya Kalangalala Mkoani Geita.Picha zote na Mary Lupamba - Acacia
Wananchi wakiwa katika banda la Acacia