Wakati Tume maalumu iliyoundwa na Serikali ikiendelea na uchunguzi juu ya ajali ya Mv Nyerere, taarifa zinaeleza kuwa aliyekuwa akiongoza chombo hicho siku hiyo hakuwa na sifa za kufanya hivyo bila uangalizi wa karibu wa nahodha.
Wakati anayetakiwa kuongoza kivuko au meli yenye hadhi ya Mv Nyerere akitakiwa kuwa na kiwango cha elimu ya masuala ya unahodha na ubaharia kuanzia Master Near Coast Deck Officer Class 4, marehemu Alan Mahatane anayedaiwa ndiye alikuwa akiongoza Mv Nyerere, alikuwa elimu ya Deck Ratings (Rating Forming Part of a Navigation Watch). Alipata elimu hiyo mwaka 2014 kutoka Chuo cha Ubaharia cha Dar es Salaam Maritime Institute (DMI).
Mmoja wa watu aliosoma nao, Salum Adam alisema licha ya kuongoza chombo hicho, kiwango chake cha elimu na majukumu ya wenye elimu hiyo haviruhusu kufanya hivyo bila usimamizi wa nahodha.
Adam ambaye ni baharia katika meli ya Mv Nyehunge inayosafirisha abiria na mizigo kati ya Nansio na Mwanza, alisema mwenye alimu kama yake anayetaka kuongoza chombo kama hicho, lazima ajiendeleze.
Social Plugin