Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BARAZA LA NNE LA WAFANYAKAZI MOI LAFUNGULIWA, WAJIVUNIA UBORA


Katibu mpya wa Baraza la Wafanyakazi wa MOI, Bwana Ngina Mitti akibadilishana nyaraka na kupongezwa na aliyekuwa Katibu wa Baraza hilo Bwana Patrick Mvungi (kulia) baada ya kumaliza muda wake wa miaka mitatu. Anayeshuhudia katikati ni Naibu Katibu mpya wa Baraza hilo Bi. Everlyne Machumu.Picha zote na Andrew Chale
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, ajali na upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dk Respicious Lwezimula Boniface (Kulia) ambaye alikuwa mgeni rasmi akimpongeza na kumkaribisha Katibu mpya wa Baraza la Wafanyakazi wa MOI, Bwana Ngina Mitti baada ya kuchaguliwa kwenye Baraza hilo la nne.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, ajali na upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dk Respicious Lwezimula Boniface (katikati) ambaye alikuwa mgeni rasmi akisoma hotuba ya ufunguzi wa Baraza hilo la Nne la Wafanyakazi wa MOI, Kushoto kwake ni Katibu mpya wa Baraza hilo Bwana Ngina Mitti na kulia ni Naibu Katibu wa Baraza Bi. Everlyne Maachumu.

Picha ya pamoja ya Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya MOI wakati wa Baraza la nne lililofunguliwa rasmi leo Septemba 22 na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, ajali na upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dk Respicious Lwezimula Boniface katika ukumbi wa mikutano wa IDDI NYUNDO, Halmashauri ya Temeke jijini Dar es Salaam.

*****

Na Andrew Chale - Dar es salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, ajali na upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dk Respicious Lwezimula Boniface amefungua rasmi Baraza la Nne la Wafanyakazi katika ukumbi wa mikutano wa IDDI NYUNDO, Halmashauri ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Dkt. Respicious Boniface amefungua baraza hilo kwa kumwakilisha Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini MOI, Bi. Zakia Meghji ambapo vikao hivyo vitafanyika kwa muda wa siku tatu huku Wajumbe kutoka katika kila idara, vitengo na chama cha wafanyakazi wa MOI (TUGHE),Wajumbe wa TUGHE mkoa huku kwa upande wa Ofisi ya Waziri Mkuu-Utumishi ikiwakilishwa na Bi.Tulia Msemwa.

Akizindua Baraza hilo Dkt. Boniface kwanza alitoa pole kwa tukio la ajali ya kuzama kwa kivuko kilichotokea kwenye Ziwa Tanganyika cha MV Nyerere na kupoteza watu wengi huku pia ametoa pole kwa Rais na Watanzania wote.

Aidha akizungumza kwenye ufunguzi huo, Dk. Boniface amesema kuwa Taasisi hiyo imenufaika na mageuzi makubwa katika kipindi cha miaka mitatu kwa huduma zimeboreka sana na zaidi ya Wagonjwa wa nje (Outpatient) zaidi ya Laki mbili wamehudumiwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2017/18.

“MOI ni ‘high Class Hospital, na huduma zetu ni bora sana ukilinganisha na Hospitali nyingine hapa Nchini na Nchi za Afrika Mashariki na Kati”,alisema Dkt. Boniface.

Dkt. Boniface amesema azma ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma zote hapa ambapo kwa hilo nchi imefanikiwa sana.

“Kwa upande wa mifupa na ajali tuko vizuri na hakuna anayekwenda nje ya Nchi. Ila kwa upande wa upasuaji wa Ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu kuna wachache wanakwenda ila Serikali inaliangalia hilo na vifaa vimenunuliwa na hakuna atakayekwenda nje ya nchi tena.

..Fedha za kununulia vifaa zilitolewa na Serikali yetu sikivu kiasi cha Tsh. 16.5 Bilioni ambazo zimeiwezesha MOI kuwa na vifaa vya kisasa vya MRI, CT-SCAN, X-ray, Utra Sound, na vingine vya kazi muhimu kwa matatizo hayo hivyo Baraza hili liwe chachu ya kukuwa kwa taasisi yetu”,lisema Dkt. Boniface.

Aidha, Dkt. Boniface ameongeza kuwa, kwa sasa wanataka kupunguza msongamano wa kwa wagonjwa wa nje wanaofika kupatiwa matibabu ya kliniki kwa kujenga jengo la kisasa huku pia mpango huo ni pamoja na kuanzisha mfumo maalum wa wagonjwa kufanya mihadi ya kuonana na Daktari kwa njia ya mtandao.

“Tunataka tuanzishe ‘propper data base’ ya uhakika yaani kila anayeingia anajulikana na anaonekana ili kuondoa ili suala la wagonjwa kuwahi namba hapa ambapo wanakuja kuanzia saa 12 alfajili hii sasa itakoma. Mfumo huu utasaidia sana hivyo kwa sasa tunajipanga kwa hilo na watalaam nimeshaongea nao”, alimalizia Dkt. Boniface.

Katika hatua nyingine, Baraza hilo liliweza kupata Katibu mpya Bwana Ngina Mitti huku Msaidizi wake Bi. Evelyne Machumu baada ya aliyekuwa Katibu wa Baraza hilo Bwana Patrick Mvungi kumaliza muda wake.

Baraza hilo la Wafanyakazi limehudhuliwa na wajumbe zaidi ya 70 huku pia pia wadau mbalimbali wakiwemo SSRA ambao walitoa mada juu ya kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi ya Jamii sambamba na Benki ya NMB ambao ni waadu wakubwa wa MOI ambao walitoa elimu na mafunzo namna ya benki hiyo inavyoweza kuwasaidia wateja wake wakiwemo wafanyakazi wa MOI.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com