Bondia Mtanzania Jonas Segu, maarufu 'Black Mamba
Bondia Mtanzania Jonas Segu, maarufu 'Black Mamba' amefanikiwa kumshinda Bondia David Rajuili kutoka Afrika ya Kusini katika pambano la ubingwa wa WBF Africa Lightweight Champion lililochezwa siku ya jana Mjini Cape Town.
Katika pambano hilo, Bondia Segu alionekana kuutawala mchezo dhidi ya mpinzani wake Rajuili, na kufanikiwa kumchakaza ndani ya raundi kumi na kuibuka na ushindi wa rekodi ya alama 19-8-2 huku mpinzani wake akishindwa kwa alama 11-9-1, pambano lililochezeshwa na Mwamuzi, Elroy Marchall.
Hili ni pambano la pili kati ya wawili hao ambapo awali Segu alipoteza ushindi dhidi mpinzani huyo kutoka Afrika ya kusini, pambano lililochezwa March 3, mwaka huu.
Huu ni muendelezo mzuri kwa Mabondia wa Tanzania kufanya vizuri katika mapambano ya nje ya nchi, baada ya majuma kadhaa yaliyopita,Hassan Mwakinyo ali ibuka na ushindi wa TKO kwa kumpiga Muingereza Sam Egginton katika raundi mbili lilofanyika England na kuiletea sifa kubwa Taifa.
Social Plugin