Wadau mbalimbali wa Mazingira wakifanya usafi kwenye ufukwe wa Coco, Kinondoni Jijini Dar es salaam katika kuadhimisha siku ya usafi duniani iliyofanyika mwishoni mwa wiki kupitia kampeni ya ‘Let’s Do it’ iliyolenga kuondoa taka kutoka kwenye mazingira ya asili.
#KINONDONI
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akizungumza na wadau mbalimbali wa Mazingira kwenye ufukwe wa Coco katika kuadhimisha siku ya usafi duniani iliyofanyika mwishoni mwa wiki kupitia Kampeni ya ‘Let’s Do it’ iliyolenga kuondoa taka kutoka kwenye mazingira ya asili.
#KIGAMBONI
Wadau mbalimbali wa Mazingira wakifanya usafi eneo la Ferry Sokoni, Kigamboni jijini Dar es salaam katika kuadhimisha siku ya usafi duniani iliyofanyika mwishoni mwa wiki kupitia kampeni ya ‘Let’s Do it’, iliyolenga kuondoa taka kutoka kwenye mazingira ya asili.
#MBEZI MWISHO - UBUNGO
Ilikuwa ni siku ya kuadhimisha siku ya Usafi Duniani iliyofanyika mwishoni kwa wiki iliyopita wakazi wa Mbezi Mwisho, Ubungo jijini Dar es Salaam walikufanyika na kufanya usafi katika maeneo yao ya biashara na majumbani kupitia kampeni ya #LetsDoit. Zoezi hili la usafi kwa Tanzania lilifanyika katika miji 33 ikiwa na Temeke, Kinondoni, Morogoro, Arusha n.k.
Kila mmoja akiwajibika kukusanya pamoja taka taka ili kuweka mazingira yao salama.
Uongozi wa Kata ya Msigani ukiwa mbele ya vifurushi vya taka taka walizokusanya pamoja na wananchi wao
Moja ya vibao vilivyowekwa mitaani kuzuia utupaji wa taka taka ovyo.
Vijana waliojitokeza katika suala la usafi wa mazingira.
Social Plugin