Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Freema Mbowe akikata utepe kwenye kitabu kuashiria uzinduzi wa sera toleo la Mwaka 2018.
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimezindua kitabu cha sera za chama hicho toleo la mwaka 2018 ikiwa na sera 12 ambazo zimezungumzia namna ambavyo chama hicho kimejipanga kuinua maisha ya mtanzania na taifa kwa ujumla.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo wa toleo hilo, Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Freeman Mbowe amesema sera za chama hicho kimelenga kuinua uchumi wa mwananchi mmoja kama ilivyokua ikitamaniwa na mwalimu Julius Nyerere kupitia sera za ujamaa na hasa kupitia azimio la Arusha la mwaka 1967.
“Mwalimu Nyerere alisema sera za Chadema zilikua sera za kuinua maisha ya watanzania, kwa hiyo chama chetu sio chama cha kutafuta uhuru, bali sera zetu zimejikita zaidi kuhakikisha kila mtanzania anakua na maisha bora, sera hizi zimelenga maeneo 12 na tutaweza kuzifanyia marekebisho mara kwa mara pindi zitakapohitajika pia ni ruhusa kunakiliwa na vyama vingine.”
Miongoni mwa vitu ambavyo sera hizo zimejikita ni masuala ya katiba, utawala bora, uchumi wa jamii, mazingira, mambo ya nje, elimu na sayansi, mambo ya siasa ya ndani, pamoja na uchumi wa vijijini.
Chanzo- EATV