Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019 imeendelea tena leo kwa michezo sita kuchezwa katika viwanja mbalimbali Tanzania, game kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union ni miongoni mwa game zilizochezwa Jumatano ya September 19 2018.
Yanga leo wameikaribisha Coastal Union inayochezewa na staa wa Bongofleva Alikiba katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Yanga wakiwa nyumbani wamefanikiwa kupata ushindi wa tatu mfululizo katika Ligi Kuu kwa kuifunga Coastal Union kwa goli 1-0, goli la Yanga likifungwa na Herietier Makambo dakika 11 kwa kutumia vyema pasi ya Ajib.
Ushindi huo sasa unaifanya Yanga kufikisha jumla ya point tisa baada ya kucheza game tatu mfululizo za Ligi Kuu na kufanikiwa kupata ushindi katika game zote, Yanga alipata ushindi wa 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar, 4-3 dhidi ya Stand United na leo 1-0 dhidi ya Coastal Union ila Coastal Union bado haijamtumia mchezaji wake mpya Alikiba katika game za ushindani.
Social Plugin