Licha ya kivuko cha Mv Nyerere kuzama majini zaidi ya saa 48 zilizopita wilayani Ukerewe, Alphonce Charahani, Mhandisi wa Kivuko cha Mv.Nyerere kilichopata ajali ya kuzama ziwa Victoriaameokolewa muda mfupi uliopita akiwa hai japo hali yake ni mbaya lakini anapatiwa huduma.
Mhandisi huyo ametolewa akiwa hai na kukimbizwa Kituo cha Afya cha Busya kilichopo katika Kisiwa cha Ukara.
Mmoja wa wazamiaji Daniel Kondoyo amesema tangu juzi Septemba 20, 2018 kilipozama kivuko hicho kila walipokuwa wakigonga walisikia mtu mwingine akigonga kwa ndani.
Baadhi ya wazamiaji wanaoopoa miili wamesema Charahani alikuwa amejipaka oili mwilini ambayo wameielezea kuwa husaidia maji yasiweze kupita katika vinyweleo.
Kandoyo amesema kutokana na hali hiyo huenda aliyekuwa akigonga kwa ndani ni Charahani.
Lakini hawezi kuongea kutokana na hali yake kuwa mbaya baada ya kukaa ndani ya maji kwa takribani siku tatu.
Tangu asubuhi leo, miili 30 imeopolewa na kufanya idadi ya miili iliyoopolewa hadi sasa kufikia 166 baada ya mili mingine 136 kuopolewa hadi jana jioni.
Miili yote iliyoopolewa imehifadhiwa katika Kituo cha afya cha Bwisya.
Miili 116 kati ya 151 iliyoopolewa baada ya kuzama kwa Kivuko cha MV Nyerere juzi Septemba 20, 2018 imetambuliwa na ndugu.
Saa 4:30 Asubuhi Septemba 22,2018
Miili mingine minne imeopolewa na kufanya jumla ya miili 26 kuwa tayari imeopolewa leo. Zoezi linaendelea.
Baadhi ya ndugu ambao jana walikataa majeneza ya kuzikia jamaa zao waliofariki katika ajali hiyo, wamebadili maamuzi yao na kuanza kudai wapewe majeneza.
Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania imetoa mchango wa shilingi milioni 10 kwaajili ya kutengeneza majeneza 100, fedha amekabidhiwa RC Mongella naye kamkabidhi Mhazini. Waziri Jenista Mhagama amesema fedha zitaingizwa kwenye akaunti ya maafa itakayotangazwa.
Saa 2:34 Asubuhi Septemba 22,2018
Miili mingine mitano imeopolewa na kufikisha jumla ya miili 21 kwa siku ya Leo na kufanya jumla ya miili 157 iliyoopolewa hadi sasa.
Saa 2:20 Asubuhi, Septemba 22
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela amesema Miili mingine 16 imeopolewa na kufanya jumla ya watu 152 waliofariki dunia kwenye ajali hiyo huku akibainisha kuwa zoezi la uokoaji linaendelea
Aidha amesema kuwa katika zoezi la utambuzi miili 116 imeshatambuliwa na ndugu zao.
Katika Hatua Nyingine Mongela amesema Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza kutolewa kiasi cha shilingi laki tano kwa kila familia ambayo imepotelewa na ndugu yake kwenye Ajali hiyo.
Social Plugin