Matumaini ya kazi ya kukinyanyua na kukigeuza kivuko cha Mv Nyerere yameanza kuonekana baada ya wataalam wa uokoaji kufanikiwa kukilaza ubavu.
Hadi jana jioni Septemba 24, 2018 kivuko hicho kilichozama mchana wa Septemba 20, 2018 kilianza kuonekana sehemu kubwa ambayo awali ilikuwa majini kutokana na vifaa mbalimbali kuingizwa majini na kutumika kukinyanyua.
Kazi ya kukinyanyua na kukigeuza kivuko hicho chenye tani 25 na uwezo wa kupakia abiria 101 na magari matatu ilianza juzi ikifanywa na wataalam kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kushirikiana na wenzao kutoka kampuni ya Songoro Marines ya jijini Mwanza.
Na Peter Saramba, Mwananchi