Mkazi wa Mwananyamala, Ahmed Mudhihiri (26), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni, Dar es salaam akikabiliwa na mashtaka matatu yakiwamo ya ubakaji na kufanya udanganyifu kuwa yeye ni mtoto wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Akisomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Caroline Kiliwa, Mwendesha Mashtaka, Neema Moshi, alidai Julai 6 katika eneo la Hoteli ya White Sands Mbezi Africana Dar es Salaam, mshitakiwa alimbaka binti (jina limehifadhiwa).
Shitaka la pili ni kuwa kati ya Juni 17 na Julai 7 mwaka huu Dar es Salaam, alidanganya kuwa yeye ni Mwamvita Makamba.
Katika shitaka la tatu, mshitakiwa alidaiwa kati ya Juni 18 na Julai 7 mwaka huu, Dar es Salaam, alijitambulisha kuwa yeye ni Edd mtoto wa CAG.
Social Plugin