Waziri wa Mambo ya Ndani mheshimiwa Kangi Lugola ameagiza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa watu wanaosambaza picha za watu waliopoteza maisha kwenye ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea juzi Septemba 20,2018.
Akizungumza eneo la tukio,Waziri Lugola ameviagiza vyombo vinavyohusika kufuatilia wanaosambaza picha hizo kwa ni kinyume cha sheria za makosa ya mtandao.
Tangu jana kumezuka tabia kwa baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii ikiwemo whatsapp,instagram na facebook wamekuwa wakisambaza picha za watu waliofariki kwenye ajali ya kivuko cha MV Nyerere kwenye magroup na wengine kupost kwenye kurasa zao kitendo ambacho ni kinyume cha sheria,utu na maadili.
Katika hatua nyingine amewaonya wanasiasa na watu wanaochukua tukio hilo na kulifanya kama mtaji wa kisiasa kuacha kufanya hivyo.
''Nawaomba wanaochukua tukio hili kama mtaji wa kisiasa waache mara moja, na waache kuchonganisha serikali na wananchi wake, kwani hatutasita kuwachukulia hatua wale wote wanaochukulia suala hili aidha kwa vitendo au maneno”, amesema Lugola.
Social Plugin