Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na Watalaamu wa Mawasiliano kutoka Shule Kuu ya Uandishi wa Habari (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam wameendesha mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali nchini kuhusu njia na mbinu za usalama na kujilinda wanapotekeleza majukumu yao.
Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyofunguliwa leo Septemba 26,2018 katika ukumbi wa VETA jijini Dodoma na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,Patrobas Katambi yamekutanisha pamoja waandishi wa habari kutoka mikoa ya Tanga,Shinyanga,Dodoma,Morogoro,Iringa,Manyara,Singida na Kilimanjaro.
Awali akizungumza Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari wa UNESCO Christina Musaroche alisema lengo la mafunzo hayo yanayoratibiwa na UNESCO ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari namna ya kufanya kazi zao kwa usalama zaidi.
Alisema madhila na vifo vya waandishi wa habari vimekuwa vikitokea wakati wakitekeleza majukumu yao kutokana na kukosa ulinzi na usalama.
Naye Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dotto Kuhenga alisema sheria za nchi zikiwa nzuri waandishi wa habari watakuwa salama huku akibainisha kuwa uwepo wa mazingira huru na salama kwa waandishi wa habari unasaidia kuwafanya wawe salama zaidi.
“Usalama wa mwandishi wa habari maana yake ni kuwepo kwa mazingira huru na salama kiafya katika kazi za mwandishi wa habari,na mazingira ya usalama ni yale ya kufanya kazi bila kuzuiwa,bila hofu ya kupata madhila kwake,familia yake na watu wanaomzunguka”,alieleza Kuhenga.
Akifungua mafunzo hayo,Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi mbali na kupongeza kazi nzuri inayofanywa na waandishi wa habari,aliwataka waandishi wa habari kuzingatia maadili ya kazi yao na kufuata sheria za nchi.
Aidha aliwakumbusha kuepuka kuandika habari kwa ushabiki huku akiwasihi kutokuwa wanyonge na watumie kalamu zao kwa haki wakizingatia usawa hali ambayo itasaidia kuchochea maendeleo katika nchi.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Dodoma,Patrobas Katambi akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu njia na mbinu za usalama na kujilinda wanapotekeleza majukumu yao leo katika ukumbi wa VETA jijini Dodoma.Kushoto ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu wa Dar es salaam Dr. Eva Solomoni,kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari wa UNESCO Christina Musaroche. Picha zote na Jumanne Juma na Kadama Malunde
Waandishi wa habari wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma,Patrobas Katambi akiwasihi waandishi wa habari kuzingatia maadili ya kazi zao.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari wa UNESCO Christina Musaroche akisoma hotuba wakati wa ufunguzi wa mafunzo/semina kwa waandishi wa habari kuhusu njia na mbinu za usalama na kujilinda wanapotekeleza majukumu yao leo katika ukumbi wa VETA jijini Dodoma
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari wa UNESCO Christina Musaroche akizungumza ukumbini.
Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dotto Kuhenga akielezea malengo ya semina hiyo kwa waandishi wa habari.
Kushoto ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu wa Dar es salaam Dr. Eva Solomoni akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Dodoma,Patrobas Katambi na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari wa UNESCO Christina Musaroche wakimsikiliza Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dotto Kuhenga.
Waandishi wa habari wakiandika dondoo muhimu wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Waandishi wa habari wakifuatilia matukio ukumbini
Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu wa Dar es salaam Dr. Eva Solomoni akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Picha ya pamoja baada ya mafunzo kufunguliwa: Mkuu wa wilaya ya Dodoma,Wataalamu wa Mawasiliano kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam,UNESCO na waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali nchini.
Picha pamoja
Mkurugenzi wa Malunde1 blog,Kadama Malunde(kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,Patrobas Katambi.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi mkoa wa Dodoma (Central Press Club) Habel Chidawali ambaye ni mwandishi wa habari wa Mwananchi Communication Ltd akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini.
Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dotto Kuhenga akitoa mada kuhusu ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari.
Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dotto Kuhenga akiendelea kutoa mada.
Mwandishi wa Habari Hamis Dambaya ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara akiwasalimia waandishi wa habari wanaoshiriki mafunzo hayo na kuwataka kujituma katika kazi zao pamoja na kuzingatia maadili ya uandishi wa habari.
Mafunzo yanaendelea..
Picha zote na Jumanne Juma na Kadama Malunde