Kufuatia ajali ya Kivuko cha MV Nyerere, Septemba 20,2018 na kuua watu zaidi ya 220,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ameivunja bodi ya ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).
Rais Magufuli ameivunja bodi hiyo ambayo mwenyekiti wake ni Brigedia Jenerali Mstaafu Mhandisi Mabula Mashauri kuanzia leo Septemba 23,2018 wakati Kamati ya Uchunguzi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea na uchunguzi wa ajali ya kivuko cha MV Nyerere ambayo imesababisha vifo vya Watanzania 224.
Social Plugin