SAKATA LA AJALI YA MV NYERERE: RAIS MAGUFULI,AVUNJA BODI NYINGINE...AMTUMBUA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI SUMATRA

Rais Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) Mhandisi Dkt. John Ndunguru na kuivunja bodi hiyo kuanzia leo Septemba 24, 2018.



Rais Magufuli amechukua hatua hiyo kufuatia ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV. Nyerere iliyotokea Septemba 20, 2018 na matukio mbalimbali ya ajali za barabarani hapa nchini yanayosababisha vifo, ulemavu na uharibifu wa mali.


Pamoja na hatua hiyo kamati ya uchunguzi ambayo itatangazwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa baadaye leo, itaendelea na uchunguzi wa ajali ya kivuko cha MV. Nyerere kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kama ilivyopangwa.


Utenguzi huu wa Rais Dkt. John Magufuli ni wa pili kuufanya tokea ilipotokea ajali ya kivuko cha Mv. Nyerere na kusababisha takribani ya watu 224 kufariki dunia kutokana na ajali hiyo.


Jana Septemba 23, 2018 Rais Magufuli aliivunja Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) iliyokuwa chini ya Brigedia Jenerali Mstaafu, Mabula Mashauri kufuatia kuzama kwa kivuko cha MV. Nyerere.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post