Makontena hayo yameshindikana kuuzwa katika mnada uliofanyika jijini Dar es Salaam. Hii inakuwa ni mara ya nne makontena hayo kushindwa kuuzika.
Akizungumza kwenye mnada huo, mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya udalali ya Yono, Scolastica Kevela amesema mnada huo umeendeshwa lakini mnunuzi hajapatikana.
Kevela amesema hadi sasa bei zinazofikiwa na wateja hazijafikia malengo waliyowekewa. Amesema wao kama madalali wataendelea kufanya utafiti wa kuwapata wateja.
Wateja wachache waliokuwa kwenye mnada huo walionekana kutaja bei lakini hakuna hata mmoja aliyefanikiwa kufikia kiwango kilichowekwa.
Social Plugin