TAARIFA KWA UMMA.
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano Awamu ya Pili
kwa mwaka 2018 wanatakiwa kuripoti kuanzia tarehe 21 hadi 30
Septemba, 2018 na hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya shule.
Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa
wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti hadi tarehe 30
Septemba, 2018 ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kuripoti, nafasi yake
atakuwa ameipoteza.
Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano
Awamu ya Pili pamoja na fomu za kujiunga (joining instructions)
inapatikana kwenye tovuti ya OR-TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz
Mwanafunzi mara upatapo jina umechaguliwa inabidi uangalie fomu ya
kujiunga na shule husika kwenye mtandao na huwajibiki kwenda kwenye
shule husika wala kupiga simu.
Imetolewa
Katibu Mkuu,
OR-TAMISEMI
BOFYA HAPA KUONA ORODHA YA WANAFUNZI WA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO AWAMU YA PILI 2018
ORODHA YA WANAFUNZI WA 2ND SELECTION SEPT 2018
Social Plugin