Habari Mpya

    Loading......

MBARONI KWA KUMTIA MIMBA BINTI YAKE....ADAI 'SHETANI ALIMPITIA'


Polisi katika Mkoa wa Mjini Magharibi wanamshikilia Muhammed Juma Muhammed kwa tuhuma za kumtia mimba binti yake wa kambo mwenye umri wa chini ya miaka 18.

Hata hivyo, kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Thobias Sedeyoka alisema jana kuwa kwa sasa yupo likizo, lakini amesikia uwepo wa taarifa za binti aliyetiwa mimba na baba yake.

Taarifa za kitendo kilichofanywa na mtuhumiwa huyo zilijulikana baada ya polisi kupatiwa taarifa na sheha wa Shehia ya Kijichi, Simba Ally Makame ambaye alipewa taarifa hizo na vijana wanaoshiriki ulinzi shirikishi. Binti huyo kwa sasa ameshajifungua.

Baada ya kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi katika Kituo cha Polisi Bububu, baba huyo alikiri kufanya kitendo hicho huku akidai kuwa “shetani alimpitia”.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com