Mbunge wa Serengeti mkoani Mara,Marwa Chacha (Chadema)amejiuzulu uanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini.
Akizungumza leo Septemba 27, 2018 Chacha amesema amechukua uamuzi huo kumuunga mkono mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli.
Amesema wakati akigombea ubunge aliahidi kuwaletea maendeleo wananchi wake lakini dhamira yake haijafanikiwa kutoka na vikwazo anavyokumbana navyo ndani ya Chadema.
Chacha amewataka wakazi wa Serengeti kumchagua mtu atakayeweza kushirikiana nao pamoja ili kuleta maendeleo kupitia CCM.
Na Beldina Nyakeke,Mwananchi
Social Plugin