Saa 10: 30 jioni Jumamosi Septemba 22,2018
Kwa mujibu wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mwasiliano, Isack Kamwelwe idadi ya miili iliyoopolewa katika ziwa Victoria baada ya kivuko cha MV Nyerere Septemba 20,2018 imefikia 209, miili 172 imetambuliwa na ndugu zao,112 tayari imeshachukuliwa na ndugu zao huku miili 37 bado haijatambuliwa na kwamba manusura ni 41.
Amesema zoezi la uokoaji linaendelea.
Tayari wadau mbalimbali wameanza kujitokeza kutoa michango mbalimbali.
Miongoni mwa wadau hao ni Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation ambayo imetoa Sh10 milioni ili zitumiwe na wafiwa katika maziko ya ndugu na jamaa zao waliopoteza maisha katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere.

Fedha hizo zimekabidhiwa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mwasiliano, Isack Kamwelwe na meneja wa Vodacom Kanda ya Ziwa, Domisian Mkama.
Baada ya kupokea fedha hizo, Waziri Kamwelwe naye amezikabidhi fedha hizo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenister Mhagama ambaye pia amezikabidhi kwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.
Mhagama ameagiza ifunguliwe akaunti maalum na mkoa huo kwa ajili ya kuhifadhi fedha zote zinazotolewa kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa ajali hiyo.
Social Plugin