Mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala, Simon Belege na mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mibako Mabubu wamenusurika kifo baada ya gari walilokuwa wamepanda kugonga ng’ombe katika mteremko wa Mlima Sekenke.
Viongozi hao walikuwa wakitokea mkoani Dodoma kuelekea Igunga, Tabora kuwahi kikao cha utekelezaji wa ilani ya CCM kitakachofanyika kesho Jumamosi Septemba 15, 2018.
Katika gari hilo, Mkurugenzi huyo alikuwa pamoja na mwenyekiti wa halmashauri hiyo, mweka hazina, Masatu Mnyoro na mwanasheria wake, Mashaka Mabula.
Majeruhi wa ajli hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Igunga mkoani Tabora wakiendelea kupatiwa matibabu.
Mganga mkuu wa hospitali hiyo, Bonaventura Kalumbete amesema Belege na Mabula ndiyo waliokuwa wamelazwa lakini baada ya kuwapatia matibabu hali zao zinaendelea vizuri na wakati wowote wataruhusiwa.
Social Plugin