MTIKISIKO CHADEMA WAHAMIA SERIKALI ZA MITAA : WENYEVITI 20 WA VIJIJI WAHAMIA CCM


Wenyeviti 20 wa vijiji wa Chadema katika jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro wamehamia CCM leo Alhamisi Septemba 6, 2018.


Mbunge wa Hai ni Freeman Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa Kambi Rasmi za Upinzani Bungeni.

Majina ya wenyeviti hao na vijiji vyao katika mabano ni, Hendry Kimaro (Lukani), Josephat Joseph (Mbosho), Comred Munuo (Kyuu), Elibariki Mbise (Rundugai), Nassor Mushi (Wari Sinde), Erasto Mushi (Kyeeri), Iddy Mtambo (Chemka), Seth Munisi (Uraa), Issa Kisanga (Kware) na Paradiso Munisi (Uswaa).

Wengine ni Emanuel Mbowe (Nshara), Simbo Mbasha (Mungushi), Bethuel Swai (Isawerwa), Godfrey Kivuyo (Jiweni), Joel Kalungwana (Nerere), Emanuel Laizer (Mlima Shabaha), Michael Kiwelu (Kambi ya Raha), Godfrey Maimu (Umoja), Witness Mwanga (Sonu).

Akizungumza na MCL Digital leo mkurugenzi wa halmshauri ya Hai, Yohana Sintoe amethibitisha kupokea barua za kujiuzulu za wenyeviti hao.

Amesema kulikuwa na wenyeviti 19 lakini mchana ameongezeka mmoja na kufikia 20. Hata hivyo mwenyekiti huyo wa 20 jina lake halijapatikana.

"Wameeleza kujiuzulu kwa ridhaa yao kutokana na kuunga mkono Serikali," amesema Sintoe.

Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amesema anawapongeza viongozi hao kwa kutumia haki yao kidemokrasia na kujiuzulu.

Sabaya amesema kwa sasa hakuna Mtanzania ambaye haoni kazi nzuri za Rais John Magufuli hivyo viongozi hao kujiuzulu wameonesha heshima kwa Rais.

"Niwapongeza kwa heshima waliyoonyesha bila kushinikizwa na mtu yoyote na mimi nawaunga mkono," amesema.

Na Mussa Juma, Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post