Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS MAGUFULI KU - DILI NA WAHUSIKA WA AJALI YA KIVUKO...ATANGAZA BENDERA KUPEPEA NUSU MLINGOTI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ameagiza viongozi wa taasisi na mamlaka zinazosimamia usafiri wa majini wahojiwe na watakaobainika kuhusika kwa uzembe wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Rais Magufuli ameagiza kuwa kufuatia ajali ya MV Nyerere Bendera ya Taifa itapepea nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia kesho Septemba 22, 2018-Katibu Mkuu Kiongozi. pic.twitter.com/eJ7oIkOPnq

View image on Twitter
Rais Magufuli ameagiza viongozi wa taasisi na mamlaka zinazosimamia usafiri wa majini wahojiwe na watakaobainika kuhusika kwa uzembe wachukuliwe hatua kali-Katibu Mkuu Kiongozi. pic.twitter.com/hlTzGCvlda

View image on Twitter

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijjazi, Dodoma leo wakati akitoa tamko rasmi la serikali kuhusu ajali ya MV Nyerere ambapo Rais ameagiza pia bendera ya Taifa itapepea nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia kesho Septemba 22, 2018.


Tamko Rasmi la Serikali Kuhusu Ajali ya MV Nyerere Lililotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijjazi, Dodoma leo.

Serikali inatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa ndugu waliofarii katika ajali ya MV Nyerere na kuwatakia majeruhi wapone haraka-Katibu Mkuu Kiongozi.
Rais Magufuli ameagiza kuwa kufuatia ajali ya MV Nyerere Bendera ya Taifa itapepea nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia kesho Septemba 22, 2018-Katibu Mkuu Kiongozi. pic.twitter.com/eJ7oIkOPnq

View image on Twitter
“Serikali inatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa ndugu waliofarii katika ajali ya MV Nyerere na kuwatakia majeruhi wapone haraka”, amesema Katibu Mkuu Kiongozi.

Idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama jana mchana Septemba 20, 2018 imefikia 131 huku uokoaji ukiendelea.

Akizungumza katika kituo cha Afya Bwisya leo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Issack Kamwelwe amesema miili 37 tayari imetambuliwa na ndugu na jamaa wakati kazi ya kuitambua iliyosalia ikiendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com