Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Shuhudia picha : MDAU WA MALUNDE1 BLOG SAID NASSORO AKIFUNGA NDOA LEO MJINI SHINYANGA

Bwana Said Nassoro Aljabry wa Tinde Shinyanga akiwa na mke wake Bi Salma Said Amour baada ya kufunga ndoa leo Mjini Shinyanga.

Mdau wa Mtandao wa www.malunde.com (Malunde1 blog) bwana Said Nassoro Aljabry wa Tinde Shinyanga amefunga ndoa na Bi Salma Said Amour wa mtaa wa Magadula kata ya Ngokolo Mjini Shinyanga.

Ndoa hiyo ya Kiislamu imefungwa leo Alhamis Septemba 20,2018 katika mtaa wa Magadula na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad.

Harusi pia itafanyika kesho Ijumaa Septemba 21,2018 nyumbani kwao na Said Nassoro Aljabry Tinde kisha kwenye ukumbi wa Mountain View Tinde.

Mwandishi wetu Kadama Malunde ametuletea picha 50 za matukio mbalimbali yaliyojiri wakati wa bwana Said akifunga ndoa na Salma leo.
Bwana Said Nassoro Aljabry wa Tinde Shinyanga akiwa na mke wake Bi Salma Said Amour baada ya kufunga ndoa leo Mjini Shinyanga.
Bwana Said Nassoro Aljabry wa Tinde Shinyanga na mkewe Bi Salma Said Amour wakifurahia baada ya kufunga ndoa leo Mjini Shinyanga.
Awali Msafara wa magari yaliyomsindikiza bwana Said kutoka Tinde yakielekea nyumbani kwao na Bi Harusi Salma katika mtaa wa Magadula mjini Shinyanga.
Gari lililombeba bwana Harusi
Mbele ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiongoza (upande wa bwana harusi) timu ya Tinde iliyokuja kuchukua mke Shinyanga Mjini
Wenyeji 'upande wa mwanamke 'wakiwapokea wageni kutoka Tinde 'upande wa mwanaume'
Katikati ni bwana Said akijiandaa kufunga ndoa
Dua ikiendelea kabla ya kufunga ndoa
Kiongozi wa dini ya Kiislam kushoto akifungisha ndoa kati ya Said na Salma
Zoezi la kufunga ndoa likiendelea
Tayari ndoa imefungwa

Bwana Harusi akisalimiana na wakwe zake na ndugu na jamaa na marafiki waliofika kushuhudia ndoa hiyo
Tunashuhudia ndoa...
Kiongozi wa dini akitoa nasaha za ndoa
Bwana Said akimwangalia mke wake bi Salma
Said akiwa na mke wake Salma
Picha mbalimbali za kumbukumbu zikaendelea kupigwa
Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Mheshimwa Azza Hilal Hamad ambaye ni dada wa bwana Said akipiga picha ya pamoja na wanandoa hao
Mheshimiwa Azza akimpongeza Said kwa kufunga ndoa 
Mheshimiwa Azza akimpongeza Salma kwa kufunga ndoa 
Kulia ni Mkurugenzi wa Malunde1 blog,bwana Kadama Malunde akipiga picha na wanandoa hao
Burudani ikiendelea baada ya ndoa kufungwa
Said akiondoka na mke wake baada ya kufunga ndoa
Said na Salma wakiwa kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda Tinde kwa ajili ya kuanza maisha ya ndoa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com