Usiku wa kuamkia leo September 9, 2018 kumefanyika shindano la Miss Tanzania kwa mwaka 2018. Mrembo Queen Elizabeth ndiye aliyeshinda taji hilo.
Queen Elizabeth kutoka Zone ya Dar es salaam alifanikiwa kuondoka na taji hilo huku akiwamwaga wenzake 19 baada ya kuingia tano bora.
Warembo hao waliulizwa maswali na aliyejibu vizuri alijichukulia maksi nyingi kutoka kwa majaji,kati ya warembo hao kuna wengine walijibu vizuri huku mmoja wao akipata kigugumizi wakati wa kujibu swali husika.
Na kati ya warembo hao warembo watatu walijibu maswali kwa lugha ya Kiingereza huku warembo wawili yaani aliyeshika nafasi ya tano na ya nne hao waliweza kujibu maswali kwa kutumia lugha ya taifa ya kiswahili huku mshindi namba tatu mpaka namba moja wakijibu kwa lugha ya kiingereza.
Warembo waliofanikiwa kufika hatua ya tano bora
Miss Tanzania mwaka 2016/18, Diana Flave akijiandaa kukabidhi taji
Katikati ni Mshindi wa Miss Tanzania mwaka 2018, Queen Elizabeth
Msanii Ruby akitumbuiza
Social Plugin