RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA DARAJA LA MTO SIBITI LINALOUNGANISHA MKOA WA SIMIYU NA SINGIDA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, Mawaziri, Viongozi wa dini na Chama akivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Daraja la Mto Sibiti lenye urefu wa mita 82 pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa km 25 katika eneo la mto Sibiti Mpakani mwa Simiyu na Singida.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, Mawaziri, Viongozi wa dini na Chama akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mitambo itakayotumika katika mradi huo wa ujenzi wa Daraja la mto Sibiti.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Sibiti, Maswa na Singida katika eneo la mto Sibiti kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Daraja la Mto Sibiti lenye urefu wa mita 82 pamoja na barabara zake unganishi zenye urefu wa km 25.
 Wanachi mbalimbali kutoka Singida, Maswa, Sibiti wakishangilia wakati wa hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo la Sibiti mpakani mwa mikoa ya Simiyu na Singida.
 Kikundi cha ngoma cha Lusanya kutoka Singida kikitumbuiza katika sherehe hizo.
Sehemu ya Daraja la mto Sibiti lenye urefu wa mita 82  upana mita 10.5 linalounganisha mikoa ya Simiyu na Singida kama linavyoonekana ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 70. PICHA NA IKULU

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post