Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazania John Pombe Magufuli amefanya uteuzi mwingine na kumteua Balozi Dkt. Aziz Ponary Mlima kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uganda.
Kufuatia uteuzi huo Balozi Mlima anatarajia kuapishwa leo Septemba 12, 2018 Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma.
Kamishna wa Polisi Diwani Athumani aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU anatarajia kuapishwa leo Chamwino Jijini Dodoma.
Social Plugin