SERIKALI KUAJIRI WATENDAJI KATA 1000

Serikali ina mpango wa kuajiri watendaji kata 1,000 ili kupunguza pengo kubwa la ukosefu wa watendaji hao katika maeneo mengi nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Joseph Kandege.


Kandege alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Tundulu Kusini (CCM), Daim Mpakate ambaye alitaka kujua ni lini Serikali itaajiri watendaji kata kwani maeneo mengi yako wazi.


Naibu Waziri huyo alikiri watendaji ni watu muhimu katika shughuli za maendeleo hivyo Serikali imeona umuhimu wa kuwaajiri ili kusukuma mbele kurudumu la maendeleo.


"Tumeomba kibali na tumepewa kuajiri watendaji kata 1,000, hivyo tuna amini tukishaajiri hao tutakuwa tumepunguza pengo hilo kwa kiasi kikubwa," alisema Kandege.

Naibu Waziri huyo alisema mpango huo utafanyika mapema kwa kuwa uhitaji wao ni mkubwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post