Mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kati ya watani wa jadi Simba na Yanga umemalizika kwa timu hizo kutoka suluhu ya bila kufungana katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ambao ni wa 86 katika historia ya timu hizo, ulikuwa mkali na wa kuvutia huku ikishuhudiwa Simba ambayo ni mwenyeji wa mchezo ikitawala katika kipindi cha kwanza na kukosa nafasi kadhaa za kufunga na kupelekea kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare ya bila kufungana.
Yanga ilianza kwa kasi katika kipindi cha pili huku wakitumia mashambulizi ya kushtukiza mara chache huku ikijihami kwa muda mwingi hali liyoifanya Simba kushambulia kwa muda wote hadi mpira unamalizika.
Kwa matokeo hayo, Yanga inafikisha alama 13 na kukwea hadi nafasi ya pili sawa na Mtibwa Sugar, huku Yanga ikisalia nafasi hiyo kutokana na uwiano mzuri wa magoli ya kufungwa na kufunga.
Simba inaongeza alama moja na kufikia alama 11 na kukwea hadi nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kuu huku Mbao Fc ya Mwanza ikiendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi kwa alama zake 14.
Social Plugin