Maofisa Waandamizi kutoka kampuni ya Tanzania Breweries Lmited (TBL Group),iliyopo chini ya kampuni ya kimataifa inayoongoza kutengeneza vivywaji ya ABInBev, wamefanya ziara ya kutembelea kambi ya wasanii watakaoshiriki katika tamasha la Fiesta 2018 iliyopo Kawe jijini Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo walipata fursa ya kuongea na wasanii hao na kuwapiga msasa kuhusiana na sera ya kampuni hiyo inayohimiza unywaji wa kistaarabu na kujadili masuala mengine ya kuendeleza sanaa sambamba na kutangaza biashara mbalimbali.
Meneja wa chapa ya bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli alisema “TBL Group Kama kampuni kubwa ya biashara za vinywaji tunalo jukumu la kukutana na makundi mbalimbali ya kijamii ,kama ambavyo tumekutana na wasanii kwa kuwa tunaamini wao ni kioo cha jamii,hivyo tumeweza kubadilishana nao mawazo mbalimbali ya kukuza Sanaa sambamba na kuwapatia mawaidha ya kufanikisha kazi zao na utumiaji wa vinywaji kistaarabu.
Meneja wa Mawasiliano ya Wateja wa TBL, David Tarimo,akiongea wakati wa ziara hiyo.
Meneja wa Masoko ya Biashara wa TBL na ABInbev Afrika Mashariki, Edith Bebwa, akiongea wakati wa ziara hiyo.
Meneja wa Mawasiliano ya Wateja wa TBL, David Tarimo, akifafanua jambo kwa wasanii
Wasanii wakimsikiliza Meneja wa Masoko ya Biashara, Edith Bebwa kuhusu shindano la kuonja bia.
Baadhi ya wasanii wakishiriki kuonja bia.
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Chege Chigunda, (kulia) akipongezwa na Meneja Masoko na Biashara wa TBL, Edith Bebwa, kwa kuibuka mshindi wa shindano la kuonja bia lililofanyika kwenye kambi ya wasanii watakoshiriki Fiesta.
Social Plugin