Kufuatia ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere iliyotokea tarehe 20 Septemba, 2018 katika ziwa Victoria, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa Temesa, Dr. Mussa Mgwatu kupisha uchunguzi.
Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliivunja Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).
Bodi hiyo iliyo chini ya Mwenyekiti wake Brigedia Jenerali Mstaafu Mhandisi Mabula Mashauri ilivunjwa kuanzia tarehe 23 Septemba, 2018 wakati kamati ya uchunguzi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea na uchunguzi wa ajali hiyo iliyotokea Mwanza.
Kutokana na ajali hiyo, Waziri Mkuu Majaliwa amesema Rais Magufuli ameagiza kuitishwa kwa zabuni ya kutengeneza kivuko kipya cha uzito wa zaidi ya tani 50 na uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 200 ili kichukue nafasi ya Mv Nyerere wakati kikiendelea na matengenezo.
Social Plugin