Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella amewapongeza wananchi kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha katika zoezi la uokoaji wa watu waliofariki katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama katika ziwa Victoria Septemba 20,2018.
Mheshimiwa Mongella ameyasema hayo muda mfupi uliopita wakati akizungumza kwenye shughuli ya mazishi ya watu waliofariki kwenye ajali ya Kivuko cha MV Nyerere ambapo amesema serikali inatambua kazi kubwa iliyofanywa na wananchi wakiwemo wazamiaji wa Ukara ambao wamejitoa kusaidia katika zoezi hilo.
Mheshimiwa Mongella kazi kubwa ya uokoaji imefanywa na wananchi ambao waliokoa watu 40 wakiwa hai, serikali na vyombo vyake wameokoa mtu mmoja pekee.
Aidha amewapongeza vikosi vyote vya uokoaji nawatu mbalimbali walioshiriki katika zoezi la uokoaji na uopoaji wa watu kwenye ajali ya kivuko hicho.