Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt Halfan Haule akizungumza katika Hafla ya kukabidhiana eneo la ujenzi wa Chuo cha VETA mkoani Rukwa.
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Adelina Macha akitoa taarifa za kuhusiana na mipango ya ujenzi ya Chuo cha VETA mkoani Rukwa.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt Halfan Haule akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa VETA Kanda VETA Makao Makuu na Viongozi mbalimbali wa Mkoa.
Kaimu Mkurugenzi wa Soko la Ajira VETA, Hildergardis Bitegera akikabidhi mchoro wa ramani ya Jengo la Chuo VETA Rukwa kwa Mkandarasi atakayejenga Chuo hicho.
Na David Edward, VETA.
KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt Halfan Haule amesema kuwa Mkoa wa Rukwa ulikuwa na uhitaji wa Chuo cha mafunzo ya Ufundi Stadi ili kuwazesha wanannchi wa mkoa huo kupata ujuzi wa ufundi kwa maendeleo ya mkoa na Taifa kwa ujumla.
Dkt Halfan Haule aliyasema wakati wa makabidhiano ya eneo la ujenzi wa Chuo cha VETA mkoani Rukwa katika hafla ya makabidhiano uliofanyika wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, amesema vijana wa Mkoa wa Rukwa ni fursa kupata mafunzo ya ujuzi na kuweza kujiajiri au kujiariwa.
Amesema wanaishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk.John Pombe Magufuli kutatua tatizo upatikaji wa chuo cha mafunzo ya Ufundi Stadi mkoani humo.
Amesema vijana watapata ujuzi wa kusindika mazao mbalimbali na maendeleo yatapatikana kupitia usindikaji ambao utaogeza thamani ya mazao.
Nae Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu naMafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Adelina Macha amesema VETA imedhamiria kujenga vyuo vya ufundi stadi kila mkoa ili kwendana na malengo ya serikali ya Tanzania ya viwanda ambavyo vitahitaji watalaam wenye ujunzi wakitokea VETA.
Amesema kuwa ujenzi wa chuo hicho kinatakiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja na kuanza udahili wa wanafunzi katika kukimbizana na ujenzi wa viwanda mkoani Rukwa ambapo ujenzi huo utagharimu zaidi ya sh.bilioni10.
Macha amesema mpango wa serikali unaolenga kuwezesha upatinakaji wa ujuzi wa ufundi stadi kwa vijana nchini ili kuwawezesha kujiajiri au kuajiriwa katika kutekeleza mpango huo nchi nzima.
Macha amesema VETA inatarajia kujenga vyuo vinne vyenye hadhi ya mkoa vitakavyojengwa katika mikoa ya Njombe,Geita,Simiyu pamoja na Rukwa.
Amesema ujenzi wa vyuo hivyo ni ishara ya kuweza kufikia malengo ya uchumi wa viwanda nchini kutokana na mkoa wa Rukwa kufanya vizuri katika Kilimo,Ufugaji pamoja na Uvuvi.
Aidha amesema kuwa ili kufikia uchumi wa kati mwaka 2025 VETA kuwawezesha wananchi kupata nguvu kazi yenye ujunzi wa kuweza kutumika katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhimiri ushindani wa soko la ajira.
Aliongeza kuwa matarajio ya serikali kuwa uwepo chuo hicho kutahamasisha maendeleo kuongeza kipato kwa wanacnhi katika mkoa wa Rukwa ambapo watafanya usindikaji wa chakula pamoja na uhifadhi wa mazao.
Amesema utafiti ulibaini kuwa shughuli kubwa za kiuchumi kwa wananchi wa mkoa wa Rukwa ni kilimo, ufugaji na uvuvi. hivyo, ujenzi wa chuo cha ufundi stadi unalenga kuwezesha na kupanua uwigo wa ajira wa kuweza kujiajiri au kuajiriwa.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Soko la Ajira VETA, Hildergardis Bitegera amesema Chuo cha Mkoa wa Rukwa kitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi 600 kwa ngazi ya kwanza hadi ya tatu katika mafunzo ya muda mrefu kwa mwaka na wanafunzi wasiopungua 900 kwa mafunzo ya muda mfupi.
Amesema kuwa katika ujenzi huo utahusisha ujenzi wa karakana zitakazofundishia mafunzo kwa vitendo katika kozi za ufundi magari,uchomeleaji na uungaji vyuma, uhudumiaji na uuzaji wa vinywaji. ufundi umeme,uandaaji na utayarishaji wa chakula, mafunzo ya ukatibu muhtasi,ubunifu wa mavazi na ushonaji wa nguo ,ufundi useremala , ufundi uashi ukarimu na utengenezaji wa chakula.