Kwa mujibu wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mwasiliano, Isack Kamwelwe idadi ya miili iliyoopolewa katika ziwa Victoria baada ya kivuko cha MV Nyerere Septemba 20,2018 mpaka sasa imefikia 224.
Kamwelwe ametoa taarifa hiyo leo Jumapili Septemba 23,2018 wakazi wa shughuli ya mazishi ya watanzania waliofariki kwenye ajali ya Kivuko cha MV Nyerere yanayoongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe mkoani Mwanza.
"Mpaka sasa watu 224 wameopolewa, kati yao wanawake watu wazima ni 126,wanaume 71,Watoto wa kike ni 17, watoto wa kiume ni 10,Waliotambuliwa ni 219 na wamechukuliwa na ndugu zao,ambao hawajatambuliwa mpaka sasa ni wanne na huyu aliyepatikana hivi punde naye bado hajatambuliwa",-Waziri Kamwelwe.
"Miili 5 ilibaki hapa wao wamesema ndugu zao wamesema wazikwe hapa hivyo tutazika watu 9,huyu mmoja aliyepatikana taratibu zitafanyika,...Tulikuta wananchi wameokoa watu 40 wakiwa hai ,sisi tumeokoa mtu mmoja ambaye ni aliyekuwa amejificha kwenye injini,tunawashukuru wazamiaji wa Ukara ambao wameshirikiana na wazamiaji wa serikali".
"Kivuko hiki kilibeba 265 ambapo uwezo wake ni kubeba watu 101 na magari matatu...Mpaka sasa wadau wamechangia shilingi Milioni 190"- Waziri Kamwelwe.