Hadi sasa ni watu 136 wamethibitishwa kufa kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere nchini Tanzania huku makundi ya uokoaji yakirejelea shughuli za kuwatafuta manusura.
Afisa mkuu wa Polisi Tanzania Simon Sirro anasema kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na mkasa huo imefikia 136, shirika la habari la Reuters linaripoti.
Inahofiwa wengine wengi bado hawajulikani waliko na kwamba huenda watu 200 wamezama.
Akizungumza katika kituo cha Afya Bwisya leo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Issack Kamwelwe amesema miili 36 tayari imetambuliwa na ndugu na jamaa wakati kazi ya kuitambua iliyosalia ikiendelea.
Kivuko cha MV Nyerere kilichozama jana mchana Septemba 20, 2018.
Kenyatta na Kagame watuma salamu za rambirambi
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametuma salamu za rambirambi kwa Rais Magufuli na Watanzania kwa jumla kutokana na mkasa huo. Amesema Wakenya wako pamoja na "ndugu zao" Watanzania kipindi hiki kigumu.
Social Plugin