Saa 7:28 Septemba 22,2018
Idadi ya watu walioopolewa ziwani yafikia 196 zoezi la uopoaji na uokoaji linaendelea.
Saa 5:22 Asubuhi Septemba 22
Mhandisi wa Kivuko cha Mv.Nyerere kilichopata ajali ya kuzama ziwa Victoria .Alphonce Charahani ameokolewa muda mfupi uliopita akiwa hai japo hali yake ni mbaya lakini anapatiwa huduma.
Imeelezwa fundi huyo alikuwa amekwama kwenye moja ya vyumba vya manahodha na alikuwa akigongagonga vitu ili waokoaji wamsikie jambo ambalo limetimia.
Lakini hawezi kuongea kutokana na hali yake kuwa mbaya baada ya kukaa ndani ya maji kwa takribani siku tatu.
Social Plugin