Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga kwa Tiketi ya CCM Mwita Waitara akizungumza Wakazi wa Kata ya Kitunda katika moja ya Mikutano yake ya Kampeni
Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde akimwaga sera za CCM Namna gani Ilanai inatekelezwa kwa Wakazi wa Kitunda wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo Jimbo la Ukonga
Mbunge wa Jimbo la Segerea , Bonnaha Kaluwa akizungumza na wakazi wa kitunda kuwataka wadumishe ujirani kw akumchagua Waitara wa CCM
Mbunge wa Ilala , Mussa Hazzan Zungu akizungumza na Wakazi wa Kitunda na kuwaomba wamchague waitara kwa kuwa ni Msikivu .
Mbunge wa Kinondoni Maulid Mtulia akiwambaia wakazi wa Kitunda Jimbo la Ukonga kuwa kuhama kwa Waitara sio shida kwnai akuanza yeye kutaka kufata Maendeleo yaliyopo CCM
Mbunge wa Ilala , Mussa Hazzan Zungu Akiserebuka na wkaazi wa kitunda kabla ya kupanda jukwaani .
Wabunge waliohudhuria Mkutano huo wakisakata rumba linalopigwa na Bendi ya TOT PLUS
Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga kwa Tiketi ya CCM Mwita Waitara Akicheza Ngoma ya Litungu kutoka Mkoani Mara
Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga kwa Tiketi ya CCM Mwita Waitara akiagana na wapiga kura waliojitokeza katika Mkutano huo
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mgombe Ubunge wa jimbo la Ukonga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwita Waitara amesema yeye sio Msaliti bali amechagua CCM ili aweze kumalizia alipoishia hususani swala la barabara , Umeme na Maji katika jimbo hilo. Waitara amesema hayo leo katika Mkutano wake wa Kampuni uliofanyika katika Kata ya kitunda.
"Naomba niwaeleze ukweli kuwa nilikuwa natumia nguvu sana katika kufanikisha mambo ya Maendeleo yenu huku kutokana na sehemu niliyokuwa hivyo sasa nimehamia huku na kila kitu sasa ni mtelezo" alisema Waitara
Alisema kuwa alikuwa anapigwa marufuku kuongea na viongozi wa CCM lakini hao ndio wenye mafungu ya Pesa na serikali jambo amblo mie nilikuwa kinyume nao kiasi cha kuanza kuniita Mimi Msaliti. Alisema kuwa hajaanza kuitwa msaliti leo kwani walimuita msaliti tangu alivyokuwa ya kuwasaidia na kuwaletea maendeleo watu ambao wamemwamini hili wapige hatua katika shughuli Zai za kila siku.
Alisema kuwa kwa sasa unaweza kuzungumza na Waziri moja Kwa moja natayari Waziri wa Nishati amemuakikishia kuwa Wakazi wote wa eneo hilo watapata Umeme Kwa gharama za Rea.
Alisema kuwa katika swala la barabara na Maji tayari linqpatiwa ufumbuzi chini ya Serikali ya Chama Cha Mapunduzi.
Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Juu ya CCM Livingstone Lusinde aliwataka watu wa ukonga wasifanye makosa kwani sasa wanachqgua Mbunge wa jimbo atakayefanya kazi na serikali na sio uchaguzi Mkuu.
Alisema CCM peke yake ndio inatekeleza ilani Kwa kupewa dhamana ya kuongoza dola hivyo wakichahua mgombea kutoka vyama vingine watakuwa wamejitafutia matatizo wenyewe
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin