Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAITARA KUONGOZA TUME YA KUCHUNGUZA AJALI YA MV NYERERE


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akionyeshana kitu na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, wakiwa katika eneo ilipozama MV. Nyerere katika kisiwa cha Ukarawa wilayani Ukerewe.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtangaza Jenerali Mstaafu George Waitara kuwa Mwenyekiti wa Tume ya kuchunguza ajali ya Mv-Nyerere na kutoa mwezi mmoja ili tume hiyo itoe majibu na mapendekezo juu ya hatua ambazo serikali inapaswa kuzichukua.

Akizungumza na wananchi wa Ukara Waziri Mkuu Majaliwa amesema serikali inaendelea na hatua za awali za kuhakikisha inawachukulia hatua waliosababisha ajali hiyo na watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Jenerali mstaafu, George Waitara.

“Hatua za awali zilishachukuliwa tulishakamata wale wote ambao waliruhusu watu kujaa, na uchunguzi unaendelea, tumeunda tume iliyojaa wataalamu na vyombo vya dola ilitubaini nani hasa muhusika, tume ina watu saba na inaongozwa na Jenerali Mstaafu George Waitara.Nimewapa mwezi mmoja ili kutoa taarifa ya tukio hilo.”

Aidha Waziri Mkuu amesema mpaka sasa michango imeshafikia milioni 310 na hazitafanya kazi yoyote badala yake watafikishiwa wafiwa ambao wamesajiliwa baada ya tukio hilo kutokea. “Mkuu wa Mkoa anaendelea kupokea michango, fedha hizi ambazo Waziri amenipa taarifa ni rambirambi za wafiwa, fedha hizo badae zote zitapelekwa kwa wafiwa, Mkuu wa Mkoa atasimamia kuhakikisha kila mfiwa aliyesajiliwa anapata salamu za rambirambi.”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com