WAZIRI LUGOLA ATEMBELEA ENEO LA AJALI YA MAGARI MANNE YALIYOGONGANA KWENYE MSAFARA KUELEKEA MKUTANO WA RAIS MAGUFULI


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akiliangalia gari la CCM Mkoa wa Mwanza lenye namba ya usajili T223 CHN Toyota Land Cruiser, lililopata ajali Kijiji cha Kasuguti Jimbo la Mwibara, wilayani Bunda Mkoa wa Mara, leo. Magari manne likiwemo moja walilopanda waandishi wa habari, yalikua katika msafara yakielekea katika Mkutano wa Rais Dkt John Pombe Magufuli, wa uzinduzi wa barabara ya kiwacho cha lami katika Kijiji cha Kisorya, wilayani humo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akizungumza na baadhi ya majeruhi wa ajali iliyojumuisha magari manne yaliyokuwa yanaenda katika Mkutano wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kwa ajili ya uzinduzi wa barabara ya kiwacho cha lami katika Kijiji cha Kisorya, Jimbo la Mwibara, wilayani Bunda, Mkoa wa Mara.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli (wa pili kulia), akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) alipokua anampongeza kwa kuja jimboni kwake Mwibara, pamoja na kumpa changamoto wanazokabiliwa nazo jimboni humo, Wilaya ya Bunda, Mkoani wa Mara, jana. Rais Magufuli alizindua barabara yenye kiwango cha lami inayojengwa kutoka Kisorya mpaka Mramba katika jimbo hilo.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli (wapili kushoto), akikata utepe kuashiria barabara ya kiwango cha lami iliyoanza kujengwa kutoka Kijiji cha Kisorya mpaka Mramba yenye kilomita 51kuzinduliwa. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola akishuhudia tukio hilo lililofanyika katika Kijiji cha Kisorya, Wilaya ya Bunda, Mkoani wa Mara, jana. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post