Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Dkt. Mwakyembe: Viongozi wa Kimila Nchini Himizeni Uzalendo na Utaifa

PIXX4
Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wazee wa Kimila wa Kimasai Bw. Amani Lukumay (Kulia) baada ya kuwasili katika Chuo cha Ufundi  cha Arusha (Arusha Technical College) kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Kimila wa Wazee hao leo Jijini Arusha.
PIXX5
 Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) akiongozana na Wazee wa Kimila wa Kabila la Maasai kuelekea mahali ambapo mkutano wa kimila unafanyika.
PIXX%2B1
Mwenyekiti wa Wazee wa Kimila wa Kabila la Maasai  Bw. Isack Lekisongo (kulia aliyenyoosha mkono) akimuonyesha Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati)  njia ambayo ilikuwa ikitumiwa na Ukoo wa Mollel kuingia  katika eneo  ambalo  hutumika kufanya mila mbalimbali za kabila hilo, eneo hilo limo ndani ya nyumba za Waalimu wa Chuo cha Ufundi Arusha (Arusha Technical College).
PIXX%2B2
Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe(Katikati) akijadiliana jambo na Viongozi na Wazee wa Kimila wa Kabila la Maasai , alipohudhuria mkutano wa kimila wa viongozi hao leo Jijini Arusha.
PIXX%2B3
Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe(Aliyekaa) akipewa fimbo na Mwenyekiti Mstaafu wa Wazee wa Kimila wa Kabila la Maasai Bw. Langidare Manapi (kulia) ikiwa ni ishara ya kukaribishwa katika kabila hilo, kabla ya kuanza kwa mkutano wa viongozi hao Leo Jijini Arusha.
PIXX%2B6
Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe(katikati) akisema jambo wakati wa Mkutano wa Kimila wa Viongozi na Wazee wa Kimasai leo Jijini Arusha, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Iddy Kimata ambaye alimuakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kulia ni Mwenyekiti wa Wazee wa Kimasai Bw. Isack Lekisongo.
PIXX%2B7

PIXX%2B8
 Viongozi na Wazee Mbalimbali wa kabila la Kimasai wakimsikiliza Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo katika Picha) alipokuwa akizungumza nao wakati wa mkutano wa kimila wa Wazee hao leo Jijini Arusha. (Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha).

Na Lorietha Laurence- WHUSM, Arusha.

Wazira wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa rai kwa Viongozi na Wazee wa Kimila nchini , kuhakikisha wanatumia nafasi walizonazo kuhimiza  uzalendo na utaifa kwa kuikumbusha jamii dhawabu ya kudumisha Utamaduni.

Hayo amesema leo Jijini Arusha katika Mkutano na Viongozi na Wazee wa Kimila wa Kabila la Wamasai,ambao hukutana mara kwa mara kujadili  mila na desturi za kabila hilo .

 Aidha Dkt. Mwakyembe amesisitiza kuwa viongozi wa kimila wana nafasi kubwa ya kujenga na kudumisha mila na desturi kwa kurithisha tamaduni hizo kwa kizazi kilichopo ili kutokupoteza tamaduni hizo muhimu.

“Kumbukeni kuwa mnanafasi kubwa ya kulea jamii yetu kwa misingi ya mila na desturi  nzuri ,kwa kuwa jamii inawasikiliza, inawaelewa na kuwaheshimu ” amesema Dkt. Mwakyembe.

Anazidi kufafanua kuwa kwa kutumia mila na desturi nzuri itasaidia kurejesha vijana ambao kwa asilimia kubwa wameadhiriwa na maendeleo ya Teknolojia na Utandawazi,hivyo kuupuza utamaduni wa mtanzania .

Vilevile Dkt. Mwakyembe amewaahidi viongozi hao kufanyia kazi changamoto wanayokumbana nayo   kuhusu eneo la kukutania lililopo ndani ya Chuo Cha Ufundi Arusha (Arusha Technical College).

Naye Mkuu wa Wilaya ya Monduli ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Iddy Kimata ameahidi kushirikiana na Mhe. Dkt. Mwakyembe katika kuhakikisha  changamoto hiyo inapata ufumbuzi ili kudumisha urithi wa Utamaduni.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Wazee wa Kimila wa Kabila la Kimasai Bw. Isack Lekisongo kwa niaba ya Wazee wenzake ameahidi kushirikiana kwa karibu na Serikali katika kuhakikisha mila na desturi zinadumishwa na kuheshimiwa .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com