Waandishi wa habari Frank Kasamwa (Star Tv) ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Simiyu (Simiyu Press Club),Samwel Mwanga anayeandikia gazeti la Mtanzania ambaye pia ni Katibu wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Simiyu na Aidan Mhando (Channel ten) wamenusurika kupoteza maisha baada ya gari walilokuwa wanasafiria kutoka mkoni Mwanza kwenda wilayani Bariadi kugongana na trekta.
Ajali hiyo imetokea jana majira ya saa tatu na dakika 20 katika kijiji cha Igegu wilayani Bariadi.
Katika ajali hiyo,waandishi wa habari hao walipata maumivu katika sehemu mbalimbali za miili yao na walipatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Simiyu.
Gari hilo ambalo ni mali ya Frank Kasamwa lilikuwa linaendeshwa na Frank Kasamwa.
Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wake wa Facebook,Samwel Mwanga ,ameandika ujumbe ufuatao.
Tunamshukuru Mungu kwa kutunusuru katika ajali baada ya gari tuliyokuwa tukisafiria kutoka Mwanza kwenda Bariadi mkoani Simiyu kugongana na trekta majira ya saa 3;20 usiku.Katika ajali hiyo hakuna mtu aliyepoteza maisha ila tumepata maumivu sehemu mbalimbali za miili yetu tulipata matibabu usiku ktk hospitali teule ya mkoa wa Simiyu.Dereva wa gari letu alikuwa ni Frank Kasamwa ambaye ni mwandishi wa habari wa Star tv mkoa wa Simiyu na mmiliki wa gari hilo,Mwingine tuliyekuwa naye ni Aidan Mhando wa Channel ten Simiyu.Mara baada ya ajali dereva wa trekta alikimbia.Ajali ilitokea ktk kijiji cha Igegu wilayani Bariadi.Tunawashukuru wote mliotoa msaada kwa namna moja au nyingine mara baada ya kupata taarifa za ajali hii Mungu awabariki nyote.
Muonekano wa gari baada ya ajali
Muonekano wa trekta baada ya ajali
Social Plugin