Waziri Mkuu wa Uganda,Ruhakana Rugunda akitembelea eneo lililoathirika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amemtumia salamu za pole rais wa Uganda Yoweri Museveni kufuatia vifo vya watu zaidi ya 40 katika ajali ya maporomoko ya udongo yaliyotokea wilaya ya Bududa.
Huu ni ujumbe aliopost Rais Magufuli katika mtandao wa Twitter
Nakupa pole Mhe. Rais Museveni na wananchi wote wa Uganda kwa kuwapoteza watu zaidi ya 40 katika ajali ya maporomoko ya udongo iliyotokea katika Wilayani Bududa. Watanzania tunaungana nanyi katika kipindi hiki cha majonzi na tunawaombea majeruhi wote wapone haraka @KagutaMuseveni
Tayari Waziri Mkuu wa Uganda, Ruhakana Rugunda amefika katika eneo la Naposho, sehemu ambayo watu na makazi yaliangamia kutokana na maporomoko ya ardhi.
na kuhaidi kuwa serikali itawapatia fedha familia zilizopoteza watu wao na kutoa misaada ya vyakula kwa watu wote wa wilaya ya Bududa.
.
Mpaka sasa Jeshi la UPDF la Uganda bado linaendelea kuwatoa watu walionusurika kwenye magofu ya nyumba zilizoporomoka kutokana na mvua kubwa ilionyesha Alhamisi katika wilaya ya Bududa, Mashariki mwa Uganda huku idadi ya maiti zilizo patikana ni zaidi ya 50.
Bado mamia ya watu hawajulikani walipo huku maafisa katika wilaya ya Bududa wakihofu kuwa idadi ya waliopoteza maisha huenda ikaongezeka.
Wakati wowote kuanzia sasa Rais Museveni anatarajiwa kufika hapa Bududa kuangalia maafa yaliotokea.Image captionMama na watoto wake 7 wakipewa misaada ya vyakula kutoka ofisi ya mwaziri mkuu wa Uganda
Wakaazi wa eneo la Manafwa na Bukalasi wilaya ya Bududa wakitoka kuzika nyumba hadi nyumba .
Daraja limepasuka katika mto Sume na mto Manafwa na sasa kuna vivuko vya muda ambavyo vimewekwa ingawa ni vya hatari sana .
Serikali imesema vikosi vya uokoaji vimefika katika eneo hilo ingawa miundo mbinu ya barabara na daraja lililoharibika zinafanya shughuli za uokoaji kuchukua muda mrefu.
Maporomoko mengine ya odongo yalishuhudiwa katika eneo hilo la Bududa yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 300 mwaka 2010.
CHANZO- BBC
CHANZO- BBC
Social Plugin