Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha :AZZA HILAL AONGOZA KIKAO CHA UWT KAHAMA..ATAKA MADIWANI,WANACCM KUZISEMEA KAZI ZA WABUNGE

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la UWT wilaya ya Kahama.Picha na Kadama Malunde.

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) amewataka Madiwani na wajumbe wa Baraza la Wanawake (UW) na Wana CCM kwa ujumla kuzisemea kazi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wabunge wao katika jamii badala ya kunyamaza na kuonekana hawafanyi lolote kwenye majimbo yao.

Azza alitoa rai hiyo jana Oktoba 16,2018 wakati akiongoza Kikao cha Baraza la Wanawake (UWT) Wilaya ya Kahama kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Mji Kahama.

Alisema madiwani na wajumbe UWT wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuzisemea kazi zinazofanywa na Rais pamoja na wabunge wao katika jamii badala ya kunyamaza na kuonekana wabunge na Chama Cha Mapinduzi kwa ujumla hakifanyi jambo lolote kwa wananchi wake.

“Zipo kazi nyingi zinafanywa na wabunge na Rais lakini hamzisemei,tunatakiwa sisi akina mama jeshi kubwa na madiwani naomba tukafanye kazi,tukieleza wananchi kazi zinazofanyika itaturahisishia hata ushindi kwenye chaguzi zijazo za Serikali za mitaa na hata uchaguzi mkuu,tufanye kazi kwa ajili ya ushindi wa CCM”,aliongeza Azza.

Katika hatua nyingine aliwataka kuimarisha vikundi vya ujasiriamali walivyovianzisha badala ya kuvihujumu akitolea mfano wa vibanda vitano vya ujasiriamali wilayani Kahama ambavyo wabunge mkoani Shinyanga Ezekiel Maige,Azza Hilal na James Lembeli walichangia mabati lakini mpaka sasa kibanda kimoja tu kinafanya kazi na mabati yaliyochangwa hayajulikani yalipo.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Katikati ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kahama,Telephora Saria akimpokea Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) alipowasili Wilayani Kahama kwa ajili ya kuongoza kikao cha Baraza la UWT wilayani humo Oktoba 16,2018 -Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la UWT wilayani Kahama.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza wakati wa kikao hicho.Kushoto ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kahama,Telephora Saria,kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Myonga.
Wajumbe wa UWT wilayani Kahama wakiwa kwenye kikao hicho.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza na wajumbe wa UWT wilayani Kahama.
Kikao kinaendelea.
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kahama,Telephora Saria akizungumza wakati wa kikao hicho.
Wajumbe wa UWT wakicheza wakati wimbo maalumu kutoka kwa msanii wa Nyimbo za Asili Mama Ushauri unaohusu kazi nzuri zinazofanywa na Mheshimiwa Azza Hilal.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akicheza muziki na wajumbe wa UWT wilayani Kahama.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akicheza muziki na wajumbe wa UWT wilayani Kahama.
Burudani inaendelea.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com