Baraza la Sanaa la taifa (Basata) limempongeza msanii Diamond kwa kuwasaidia watu wa eneo lake la Tandale jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa leo Oktoba 5, 2018 na Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza katika sherehe za kuzaliwa msanii huyo zinazofanyika viwanja vya Maguniani Tandale.
Amesema ni nadra kwa watu waliofanikiwa kukumbuka walikotoka kitendo cha kuwasaidia wana Tandale kimeonyesha utofauti wake.
Katibu Mtendaji huyo ametoa pongezi hizo za aina yake kwani alipopanda jukwaani alianza kwa kuchana mistari ya kumpongeza Diamond.
Social Plugin