Wanafunzi wapatao 2,397 wamepangiwa mikopo katika awamu ya pili ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019.
Idadi hiyo inafanya jumla ya Wanafunzi wa elimu ya juu wapatao 27,929 kati ya wanafunzi 40,000 wa mwaka wa kwanza kupangiwa mikopo hadi leo.
Taarifa
iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa
Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Abdul-Razaq Badru imesema kuwa idadi ya
wanafunzi waliobaki wapatao 12,071 watapangiwa mikopo katika awamu inayofuata ili kukamilisha idadi iliyopangwa.
Orodha ya majina ya wanafunzi hao 27,929 waliokwishapangiwa mikopo inapatikana kwenye tovuti hii na itatumwa kwenye vyuo husika kwa ajili ya hatua zaidi za kukamilisha malipo ya mikopo hiyo.
Imetolewa na:
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Social Plugin