Kamanda wa Polisi Mkoani Lindi, Prudeciana Protas amethibitisha kukimbia kwa dereva wa gari aina ya lori, mali ya kampuni ya Dangote ambalo limesababisha ajali iliyopelekea vifo vya watu 5.
Kamanda huyo amesema kuwa ajali hiyo imetokea jana majira ya asubuhi ambapo kwa mujibu wa mashuhuda, chanzo cha ajali ni gari hilo la mizigo kuacha njia yake.
“Tukio lilitokea saa kumi na mbili kasoro robo asubuhi, ndani ya 'hiace' ambayo ilikuwa na watu 6 ambapo watano kati yao walifariki. Chanzo cha ajali ni dereva wa roli kuhama upande wake, na baada ya kusababisha ajali dereva alikimbia na tunamtafuta, tunamuomba ajitokeze.” Amesema Kamanda Prudeciana
Katika ajali hiyo watu watano walifariki na mmoja kujeruhiwa baada ya 'Hiace' yenye namba T 760 CUZ iliyokuwa ikitokea Kiranjeranje kuelekea Lindi mjini kugongwa na gari ya mizigo ya kampuni ya Dangote yenye nambari T-515 katika kijiji cha Likahakwa mkoani Lindi
Social Plugin