WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani kulia akizundua mradi wa umeme wa gharama nafuu (REA awamu ya tatu) kwenye Kijiji cha Katurukila wilayani Kilombero mkoani Morogoro wakati wa ziara yake kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kilombero James Ihunyo akishuhudia
WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani kulia akizindua mradi wa umeme wa gharama nafuu (REA awamu ya tatu) kwenye Kijiji cha Katurukila wilayani Kilombero mkoani Morogoro wakati wa ziara yake
WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa kwenye Kijiji cha Katurukila wilayani Kilombero mkoani Morogoro mara baada ya kuzindua Rea awamu ya tatu
WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa kwenye Kijiji cha Katurukila wilayani Kilombero mkoani Morogoro mara baada ya kuzindua Rea awamu ya tatu
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la Tanesco Mhandisi Theodory Bayona ambaye pia ni Meneja Mwandamizi wa Usambazaji na huduma kwa wateja akizungumza katika uzinduzi huo
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani kulia akimsikiliza kwa umakini Meneja wa Shirika la Tanesco mkoani Morogoro Mhandisi Hassan Saidi wakati wa ziara yake
****
WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewaagiza Mameneja wa shirika la Umeme (Tanesco) kote nchini kuhakikisha wanakata huduma ya umeme kwa wadaiwa sugu ikiwemo sekta binafasi na serikalini.
Dkt Kalemani aliyasema hayo wakati wa ziara yake wilayani Morogoro iliyokuwa na lengo la kutembelea maeneo yanayozalisha umeme ikiwemo Kidatu ambako uzalishaji wa umeme ni 204 mw.
Licha ya kutembelea eneo hilo lakini pia alizindua mradi wa umeme wa gharama nafuu (REA awamu ya tatu) kwenye Kijiji cha Katurukila wilayani Kilombero mkoani Morogoro.
Alisema kwamba hatua hiyo inaweza kuwa mwarobaini wa kuweza kusaidia kukusanya madeni hayo ambayo yamekuwa kwa muda mrefu na hivyo kupelekea kukwamisha malengo yao waliojiwekea.
Aidha alisema kwamba haiwezekani shirika hilo likawa linawadai watu fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kwenye kutekeleza shughuli za kimaendeleo na kuweza kuwafikia wananchi wengi huku wakiacha kuwachukulia hatua ambazo zinaweza kusaidia kupata ufumbuzi wake.
“Ndugu zangu mameneja wa mikoa hakikisheni mnawakatia umeme wadaiwa wote sugu kwenye maeneo yenu wakiwemo wale wa sekta binafasi na serikali kwani hii ndio njia inayoweza kuwasaidia kukusanya madeni hayo “Alisema Dkt Kalemani.
Akizungumzia kitengo cha huduma kwa wateja ndani ya shirika hilo Dkt Kalemani alisema ni muhimu watumishi wa kada hiyo wakabadilikana kitabia kwa sababu imedodira sana na kwenye maeneo mengi hazifanyi kazi zao ipasavyo.
“Ukatakuta wateja wanapiga simu haipokelewi wakati watu wanaohusika nacho wapo hivyo kuanza sasa sipendi kusikia simu ikipigwa haipokelewi mameneja hakikisheni watu wa namna hiyo mnawachukuliwa hatua”Alisema.
“Lakini pia ikibidi mtoeni yupo ndani ya uwezo wenu lakini kama anamajibu mabaya wachukulieni hatua…. Haiwezekani mtu anapiga simu unamwambia huu sio masaa ya kazi juzi manyara nilipiga simu nikaambiwa kwamba haya sio masaa ya kazi huyu mtu bado namtafuta kwani huwezi kuwa na biashara nzuri kama mtu anayekutana na wateja wao hatekelezi wajibu wake”Alisema Waziri Dkt Kalemani
Awali akizungumza katika ziara hiyo Meneja wa Shirika la Tanesco Kanda ya Kati Mhandisi Atanausus Nangali alisema mradi huo wa gharama nafuu ni mradi wa ubunifu wa miundombinu ya gharama nafuu wa majaribio uliojengwa kupitia Rea na kugharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Alisema kwa Tanzania mradi huo umefanyika kwa wilaya mbili ambazo ni wilaya ya Mbozi wilayani Mbeya na Kilombero mkoani Morogoro kwa mkoa wa Morogoro mradi wa LCD ambao ulitekelezwa na mkandarasi NAMIS Corparate Limited chini ya usimamizi wa Tanesco uliandaliwa kujenga njia za umeme zenye urefu wa kilomita 137.7 na msongo wa kati.
Alisema pia kilomita 55.4 za umeme mdogo na kuweka mashine umba 320 na kuunganisha wateja 5731 kati ya hao wateja 5637 wa njia moja na wateja 94 wa njia tatu katika kutekeleza mradi huu mkandarasi alipewa jukumu la kujenga mifumo ya kusambaza umeme kwa gharama ya dola za kimarekani milioni 2.4 huku zifaa vyote vikiletwa na kampuni ya Rea.
Social Plugin