Ushawishi huo umetoka kwa straika wa Azam FC, Donald Ngoma ambaye amesema Chirwa ni chaguo sahihi kutua klabuni hapo.
Chirwa kwa sasa anadaiwa kuvunja mkataba na timu yake ya Nogotoom ya Misri kwa kile kilichodaiwa timu hiyo kushindwa kukidhi mahitaji yake kwenye mkataba, ikiwa ni miezi michache tangu alipoachana na Yanga, aliyoitumikia kwa misimu miwili mfululizo.
Alando amesema ujio wa Chirwa hapa nchini hauhusiani na suala lolote juu ya kusajiliwa na Azam FC isipokuwa anaenda kule kwa sababu ya uhusiano wake na Ngoma.
“Uwezo wa Chirwa uwanjani ni mkubwa na ni wazi ana uwezo mkubwa kufanya lolote na kila mtu angemtamani isipokuwa sisi kama uongozi hatujafanya naye mazungumzo zaidi ya kocha Hans na ndugu yake Donald,” alisema meneja huyo.
Musa Mateja, Dar es Salaam