Mtangazaji wa Idhaa ya Sauti ya Kiswahili (DW) ya Ujerumani, Isack Gamba amefariki dunia akiwa nchini humo.
Taarifa za awali za kifo cha mtangazaji huyo Mtanzania zinadai amekutwa amefariki dunia nyumbani kwake leo Alhamisi Oktoba 18, 2018.
Mmoja wa marafiki zake waliozungumza na Mwananchi kwa njia ya simu kutoka Ujerumani amesema jana Gamba hakuonekana kazini pamoja na juzi Jumanne.
“Hata leo Alhamisi, hakuonekana kazini asubuhi, ndipo tukaamua kwenda kutoa taarifa polisi, waliofika nyumbani kwake na kuvunja mlango wakamkuta Gamba ameshafariki dunia.”
Akiwa nchini, Gamba amewahi kufanya kazi vyombo mbalimbali vya habari ikiwamo Redio Uhuru, RFA, ITV na kabla ya kwenda Ujerumani alikuwa Radio One.
Chanzo- Mwananchi
Social Plugin