HISTORIA YA MAREHEMU ISAAC NYAGABONA MUYENJWA GAMBA.
Ratiba Kwa Ufupi
Jumatatu Alfajiri - Kupokea Mwili Airport
Jumatatu Kuanzia Saa Tano - Ibada na Heshima za Mwisho, Lugalo Hospital.
Jumatano - Mazishi Bunda.
A: KUZALIWA
Marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba, ni mtoto wa 12 kati ya watoto 13 wa familia ya marehemu mzee Elizaphan Munyenjwa Maribwa.
Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba alizaliwa january 19th 1970 wilayani bunda-mjini.
B: KUSOMA NA KAZI
Marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba, alipata elimu yake ya msingi, katika shule ya msingi Kabalimu iliyoko mjini Bunda kuanzia mwaka 1978 nakuhitimu mwaka 1984. Baada ya hapo, aliendelea na masomo ya Sekondari katika shule ya sekondari Majengo Moshi kuanzia mwaka 1985 hadi mwaka 1988 na baadaye kuendelea na masomo ya A Level katika shule ya Old Moshi kuanzia mwaka 1989 hadi mwaka 1991.
Kisha akajiunga na mafunzo ya jeshi kwa mujibu wa Sheria katika jeshi la kujenga Taifa (JKT) mwaka 1991. Baadaye alipata mafunzo ya uandishi wa Habari katika Radio Sauti ya Injili ya Mjini Moshi.
Marehemu alifanikiwa kuhitimu elimu yake ya shahada ya Mass communication katika chuo cha Tumaini jijini Dar es Salaam mnamo mwaka 2010.
Marehemu alianza kufanya kazi kwa muda wa takribani miezi sita akiwa Arusha katika Radio 5, na ndipo kwenda kujiunga na kituo cha utangazaji cha Radio Free Africa (RFA) Mwanza mwaka 1997's mpaka mwaka 2003, Kisha akajiunga na Radio Uhuru ya jijini Dar es Salaam mwaka 2004.
Marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba mwaka 2005 alijiunga na kampuni ya IPP Media katika kituo chake cha habari cha Radio One na ITV hadi mwaka 2015 alipo hamia katika shirika la utangazaji Ujerumani la Deutsche Welle (DW) ambapo mauti ilimfika akiwa huko.
C: MAISHA YA KIROHO
Marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba alikuwa ni mshiriki wa Kanisa la wa adventista wa sabato Mwenge jijini Dar es Salaam.
D: UGONJWA NA UMAUTI
Marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba hakuwahi kuuguwa ugonjwa wowote wa kuaminika zaidi ya kukutwa akiwa amefariki chumbani kwake tarehe 18 october2018 siku ya Alhamisi.
Baada ya uchunguzi wa hospital Ujerumani, imegundulika kuwa kilicho sababisha kifo chake ni kuvuja kwa damu kwenye ubongo (Brain Hemorrhage) yaani Presha ya Damu.
E: MAHUSIANO
Marehemu hakuwahi kuoa na hana Mtoto/Watoto wanao tambulika na familia.
F: SHUKRANI
Familia ya marehemu Mzee Elzaphan Muyenjwa Maribwa, inatoa shukrani kwa Watu binafsi na taasisi kama ifuatavyo hapa chini.
i.Shirika la utangazaji la idhaa ya Kiswahili Ujerumani DW:
Familia inashukuru uongozi wote wa DW kwakuguswa na kushtushwa sana na kifo cha Marehemu na kwajitihada zao walizofanya katika kufuatilia sababu za kifo cha Marehemu. Napia kukubali kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka Bonn Ujeruman hadi nyumbani kwao Bunda.
ii.Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani:
Familia pia inashukuru Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani kwa jitihada zao kwa kuhakikisha kwamba mwili wa Marehemu Isaac Muyenjwa Gamba unasafirishwa kurudi nyumbani kwao Tanzania.
iii.Uongozi wa IPP Media na wafanyakazi wake:
Familia inatoa shukrani kwa Uongozi wa IPP Media na wafanyakazi wake kwa ushirikiano wao katika maandalizi ya kuuaga mwili wa Marehemu Isaac Munyenjwa Gamba.
iv.Wananchi wote wa Dar es Salaam, Bunda na watanzania kwa ujumla:
Familia inatowa shukrani zao za dhati kwao kwakuguswa kwa masikitiko makubwa na Msiba wa ndugu yetu mpendwa Isaac Nyagabona Muyenjwa
Chanzo-BBC