Gazeti la Jamhuri limeandika kuwa, Mfanyabiashara maarufu nchini aliyekuwa ametekwa, ana microchip mwilini iliyomsaidia kurekodi matukio yote yaliyokuwa yakifanyika tangu kutekwa kwake katika Hoteli ya Colosseum, jijini Dar es Salaam.
"Kweli Mo alifanya uwekezaji wa maana kuwekewa microchip mwilini mwake. Wakati anaweka kila hicho miaka 10 iliyopita, hakujua kuwa kitakuwa na faida kwa kiwango hiki ila kifaa kimemwokoa kwani kimerekodi mazungumzo yote na wakati mwingine kupiga picha baadhi ya maeneo alikowekwa kulingana na positioning."
Gazeti hilo limedai kuwa, taarifa hizo zilizorekodiwa zipo London, Uingereza, New York, Marekani na Jo-burg, Afrika Kusini katika mitambo ya kuhifadhia kumbukumbu (servers).
Jamhuri imedai kuwa, hapa Tanzania kuna matajiri zaidi ya 35 waliofungwa kifaa hicho. Ilielezwa kuwa, matajiri wengi barani Afrika walianza kujilinda kijitali baada ya kuanza kwa vurugu za ugaidi mwanzoni mwa miaka ya 2000. Ili elezea kuwa, Teknolojia ya microchip inatumia satellite badala ya GPS kuepusha alive na microchip asipoteze mawasiliano muda wote.
Social Plugin